Category: Kitaifa
NHC yakaidi amri ya Mahakama
Uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) unatuhumiwa kukaidi amri ya Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyotolewa miaka 13, iliyopita ikiwaamuru kumrudisha katika nyumba au kumlipa afisa mstaafu wa Serikali ya China, Li Jianglan, baada ya kumwondoa bila kufuata taratibu….
Moto wawaka Tunduma
Serikali imewasha moto wa aina yake katika Mji wa Tunduma baada ya kuwapa wiki moja wananchi waliojenga katika eneo la mpaka (no man’s land) kuhamisha mali na kuvunja nyumba zao kwa hiyari, JAMHURI linathibitisha. Uamuzi wa Serikali umekuja wiki moja…
KKKT kuchunguza tuhuma za ushoga
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, limeunda kikosi kazi kuchunguza tuhuma za baadhi ya Wachungaji na Wainjilisiti wa kanisa hilo, wanaotuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Kikosi hicho kimeundwa wiki iliyopita na Askofu wa Kanisa…
Elimu ya kemikali tatizo mkoani Geita
Mkoa wa Geita ni miongoni mwa mikoa ambayo kuna migodi ya dhahabu, ambayo pia inahusisha matumizi ya kemikali bila kufuata masharti kama yalivyoainishwa na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Kumekuwapo na matumizi ya kemikali hatarishi katika mazingira bila kujali…
Faru John wamemnywa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amekalia kuti kavu baada ya taarifa kuanza kuvuja na kuonesha kuwa aliwasilisha pembe za faru ‘feki’ kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Taarifa za uhalisia wa pembe alizowasilisha zinaacha maswali mengi baada ya…
Wauza ‘unga’ wabuni mbinu
Wafanyabiashara haramu ya dawa za kulevya nchini wamebuni mbinu mpya za kukwepa kukamatwa na vyombo vya dola wanapofanya biashara hiyo, JAMHURI limebaini. Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebainisha kuwa wafanyabiashara wamefikia hatua hiyo kwa nia ya kusafirisha ‘mizigo’ bila kukamatwa. Kwasasa…