Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na liyekuwa mweyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo, Mama Anna Mgwira ametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Anna Mgwira ametangaza uamuzi wake huo, leo katika Mkutano Mkuu wa umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo mjini Dodoma.

“Nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa mbele” amesema RC Anna Mgwira.

Anna Mghwira ambaye alikuwa mgombewa wa kiti cha urais kupitia tiketi ya chama cha ACT- Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, aliteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli mwaka huu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ili kuziba pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadick aliyejiuzulu nafasi hiyo.

Kufuatia uteuzi huo, Chama cha ACT- Wazalendo kilimvua nafasi yake ya uenyekiti katika chama hicho ambapo alibakia kuwa mwanachama wa kawaida.

 

Please follow and like us:
Pin Share