Category: Maoni ya Mhariri
Tusikubali kuibiwa tena
Kwa miezi miwili sasa tumekuwa tukishuhudia taarifa zenye kupasua mioyo ya Watanzania wanaoishi kwa mlo mmoja na kuishi katika umaskini wa kutupwa. Watanzania wamesikia taarifa za nchi hii kuibiwa wastani wa Sh trilioni 108 kupitia makinikia yaliyosafirishwa nje ya nchi…
Watanzania tushikamane
Katika toleo la leo tumechapisha taarifa zinazoonyesha kuwa Serikali imechukua hatua ya kurekebisha kasoro zilizodumu kwa takriba miaka 20 katika sekta ya madini. Serikali imepeleka bungeni miswada ya sheria tatu zenye lengo la kupitia mikataba ya sasa ya madini na…
Wanaobakwa wahurumiwe
Hivi karibuni Rais John Pombe Magufuli ametoa msimamo kuwa chini ya uongozi wake mwanafunzi yeyote atakayepata mimba akiwa shuleni; shule za msingi na sekondari atafukuzwa shule. Rais Magufuli amesema wazi kuwa watakaohusika kuwapa mimba watoto nao watafungwa kwa mujibu wa…
Uzalendo si kuwabeba wasiokuwa na sifa
Miongoni mwa habari zilizopewa umuhimu wa juu katika matoleo yaliyopita ya Gazeti la JAMHURI, zilihusu zabuni za mabilioni ya shilingi kwenye Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini. Mradi huo ulio chini ya Wakala wa Nishati Vijijini…
Ni wakati sahihi kuachana na wanyonyaji
Katika mambo ambayo yamekuwa kero kwa Watanzania kwa kipindi kirefu, ni pamoja na suala la mikataba ya siri ya uchimbaji madini, mikataba ya ufuaji umeme baina ya mashirika na Shirika la Umeme nchini (TANESCO). Suala la usiri katika mikataba ya…
Tusipuuze mauaji ya Kibiti
Leo gazeti hili la JAMHURI limechapisha taarifa za Jeshi la Polisi kutangaza orodha ya watu 11 wanaotuhumiwa kufanya mauaji huko wilayani Rufiji. Mauaji haya yanafanywa kwa utaratibu wenye kutia shaka. Hawauawi wananchi wa kawaida. Wanauawa viongozi. Hadi sasa viongozi wapatao…




