JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Maoni ya Mhariri

Hivi haya ya Tanzania ni ‘majiji’ au ni ‘mazizi’?

Wiki iliyopita Tanzania imeongeza jiji jingine kwenye orodha yake. Arusha imeungana na majiji mengine yaliyoitangulia- Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Tanga. Mamilioni ya shilingi yametumika kwenye uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wa ziara yake mkoani Arusha. Kitu cha maana zaidi kilichofanywa na Rais Kikwete kwenye ziara hiyo ni uzinduzi wa Chuo cha Nelson Mandela, kitakachosaidia kuibua na kuendeleza vipaji katika fani ya sayansi hapa nchini.

Bunge lisipuuze kilio cha wafanyakazi

Leo Bunge la Jamhuri ya Muungano linaanza mikutano yake mjini Dodoma, huku wafanyakazi na Watanzania kwa jumla wakitarajia kusikia limeifanyia marekebisha ya Sheria mpya ya Mafao ya wanachama wa Mifuko ya Jamii.

Watanzania tusikubali udini utupore amani

Watanzania kwa jumla tuna kila sababu ya kuhakikisha dhana ya udini haipati mwanya wa kuvuruga ustawishaji na udumishaji wa amani, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo nchini.

Tumuenzi Nyerere kwa kufifisha udini

Oktoba 14, mwaka huu, mwasisi na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ametimiza miaka 13 tangu afariki dunia. Siku ya kuadhimisha kifo chake, tumeusikia ujumbe mzito kutoka serikalini, taasisi mbalimbali na watu binafsi, wote wakiahidi kumuenzi kwa mema yote aliyoyatenda.

Bomu la elimu litailipukia Tanzania

Mwishoni mwa wiki, gazeti la Serikali la Daily News limekariri kundi la wanafunzi wakitoa kilio kueleza masikitiko yao kuwa wameshindwa kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), na hivyo kuna wasiwasi kuwa hawataingia vyuoni mwaka huu. Kundi kubwa la wanafunzi waliohojiwa ni la watoto kutoka familia masikini.

Rushwa uchaguzi CCM inatisha

Uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaelekea ukingoni. Tayari viongozi wa nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya mashina hadi Taifa wameshapatikana. Tunawapongeza waliochaguliwa. Lakini pongezi zetu za dhati kwa kweli tunazielekeza kwa wale waliochaguliwa bila kujihusisha na vitendo vya rushwa.