JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Makala

Miradi kuineemesha Mtwara

Itakuwa si haki kukaa bila kuona na kuthamini mchango wa serikali katika kuleta maendeleo ya nchi. Kwa namna moja ama nyingine, mambo mengi ya kimaendeleo yamekuwa yakifanyika siku hadi siku hapa nchini kwetu, ambayo ukiyatazama yameendelea kutupa sifa sisi kama…

Ndugu Rais magonjwa ni mengi, kwanini tukazanie moja?

Ndugu Rais, Baba Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania, Emmaus Mwamakula, malango yake yabarikiwe. Huyu ni kiongozi mkuu wa dini katika nchi yetu ambaye bila kujali kama atahusishwa na makundi fulani fulani, amesimama hadharani na kuitetea haki….

Kwa nini Waislamu nchini wawe chini ya Bakwata? (3)

Katika sehemu ya pili ya makala hii nilieleza kuwa Bakwata ni chombo cha kudumu kilichoundwa mwaka 1968 kuratibu, kusimamia na kuongoza shughuli zote za Waislamu nchini Tanzania (Tanzania Bara) kwa lengo la kutekeleza wajibu wa Waislamu wa kuendeleza na kuimarisha…

Corona inabisha hodi, yafaa kuamka

Nimesimuliwa jinsi abiria wa ndege aliyekaa pembeni ya Mchina kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza alivyoingiwa hofu ya kuambukizwa homa ya corona – COVID-19 – akaamua kusoma gazeti tangu ndege inapaa hadi inatua Mwanza, akiamini gazeti litamkinga kuambukizwa. Hii simulizi…

Ni haki yako kuijua Sheria ya Mirathi

Mpenzi msomaji, ungana nami katika safu hii ufahamu maana ya mirathi. Mirathi ni mali iliyoachwa na mtu aliyefariki dunia kwa ajili ya kurithishwa warithi wake halali. Sheria imeweka taratibu maalumu zinazoongoza ukusanyaji, uangalizi, usimamizi, ugawaji na umiliki wa mali hizo…

Je, jicho lako la tatu linaona?

Unaweza kuwa na macho mawili bila maono. Unaweza kuwa na macho mawili yanayotazama lakini bila jicho la tatu linaloona: jicho la akili, jicho la moyo na jicho la imani. Kipindi cha siku 40 cha kufunga ni kipindi cha kufanya toba…