Na Happy Lazaro, Arusha
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha leo limetangaza rasmi majina ya wagombea wa nafasi za udiwani kwa Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni na kupitia taratibu za chama.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za chama hicho jijini Arusha, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipurani Ramsey, amesema uteuzi huo umezingatia vigezo vya uadilifu, uzoefu wa uongozi, uwezo wa kushirikiana na wananchi pamoja na historia ya utumishi katika chama.
“Tumekamilisha mchakato wa ndani kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni za chama. Wagombea hawa wameshinda kutokana na kuaminiwa na wanachama kupitia kura za maoni na uthibitisho wa vikao vya juu vya chama,” amesema Ramsey.
Ameongeza kuwa wagombea hao wanatarajiwa kwenda kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao, huku akisisitiza mshikamano na kampeni za kistaarabu.
Aidha alitaja orodha ya wagombea walioteuliwa Jimbo la Arusha Mjini lenye kata 25 ni Kata ya Engutoto -Hamza Juma, Kata ya Moivaro- Philemon Mollel, Kata ya Levolosi -Abbas Mustafa, Kata ya Themi -Melace
Kata ya Engutoto -Hamza Juma, Kata ya Moivaro- Philemon Mollel, Kata ya Levolosi -Abbas Mustafa, Kata ya Themi -Melace Kinabo, Kata ya Terat -Julias Sekeyani
Kata ya Ngarenaro -Abdulazizi Chende (Dogo Janja), Kata ya Olorien-Zacharia Mollel, Kata ya Kati -Abdulrasul Tojo.
Pia Kata ya Osunyai-Elirehema Nnko,
Kata ya Kaloleni- Maximilian Iranghe, Kata ya Sekei-Emanuel Kisira, Kata ya Lemara -Matuyani Laizer, Kata ya Unga-limited -Mahamudu Omari, Kata ya Sokoni one- -Muksini Juma, Kata ya Sombetini -Godfrey Kitomari, Kata ya Sinoni-Peter Inyasi, Kata ya Olmoti- Robert Komani, kata ya Moshono-Siriel Mbise, Kata ya Eleray -Losioki Laizer, Kata ya Kimandolu Abrahamu Mollel,
Kata ya Muriet -Credo Kifukwe.
Kata ya Baraa-Jacob Mollel, Kata ya Daraja mbili -Prosper Msofe, Kata ya Sakina Hillar Mollel na Kata ya Olasiti uhakiki bado unaendelea.
Ramsey ametumia nafasi hiyo kuwataka wanachama na viongozi wa CCM kuungana kuanzia ngazi ya mashina, tawi na kata ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa wagombea wote walioteuliwa.
