Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni muhimu kukuza ushirikiano na mshikamano wa vyama sita rafiki vya ukombozi Afrika.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mizengo Pinda alisema hayo akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano mkuu maalumu wa vyama sita rafiki vya ukombozi kusini mwa Afrika mjini Gauteng, Afrika Kusini.

Vyama hivyo ni ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), ZANU PF (Zimbabwe), FRELIMO (Msumbiji) na CCM. Pinda alisema mustakabali wa mataifa ya Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji, Zimbabwe, Angola na Namibia unategemea kwa kiasi kikubwa uhusiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi wake.
Akitoa salamu za CCM alisema vyama rafiki vinawajibika kuhakikisha vinadumisha mshikamano, maadili ya ukombozi, na misingi ya haki, usawa na maendeleo jumuishi kwa wananchi wote kama ishara ya kutekeleza kwa vitendo Ajenda 2063 ya Afrika tuitakayo.
Pinda alisema ni muhimu kujumuisha vijana katika kila hatua ya harakati za kisiasa na maendeleo ya jamii ili kujenga kizazi cha vijana wazalendo, wenye ufahamu wa historia ya vyama hivyo kama ilivyokuwa kwa waasisi wa vyama hivyo.

“Maendeleo ya Afrika yatakuja kwa dhamira ya dhati ya kulinda, kudumisha na kuendeleza misingi ya waasisi wetu ikiwa vijana watakuwa sehemu ya maendeleo hayo,” alisema.
Pinda alisema mkutano huo ni muhimu katika kukutanisha viongozi na akatoa rai wautumie kujenga fikra za vijana kwa ajili ya kuendeleza mambo mazuri yaliyoasisiwa na waasisi na asasi 76 za ndani na 12 za kimataifa zimepewa kibali cha kuwa waangalizi wa uchaguzi.
“Tume ina matumaini makubwa ya kufanikisha uchaguzi huu kwa kutegemea ushiriki wenu katika hatua zote zilizosalia kufikia siku ya uchaguzi, imani hii inatokana na ushirikiano mliouonesha wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura,” alisema.

