





Harambee hiyo, iliyofanyika Agosti 12, 2025 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ilihudhuriwa na viongozi wa serikaki wanachama wa CCM, wakereketwa, wafanyabiashara, watu maarufu na wa Tanzania wapenda maendeleo wakiwemo wanasiasa waliotia nia katika uchaguzi ujao wa 2025.
Kupitia tukio hilo, zaidi ya Shilingi bilioni 86.3 zimekusanywa kwa njia ya fedha taslimu na ahadi za michango, zikiwa ni sehemu ya maandalizi ya shughuli za kampeni za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ambapo lengo ni kukusanya bilioni 100.


