Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Albet Chalamila amewataka madiwani na viongozi mbalimbali wanapo kwenda kwenye mabaraza yao wawe wanaingiza hospital binafsi kama Hospital ya Shifaa ili iwe sehemu
yao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, wakati wa siku ya pili ya ziara yake ya kikazi alipotembelea Hospitali ya Shifaa iliyopo Kata ya Ananasif, Wilaya ya Kinondoni, kwa lengo la kukagua huduma zinazotolewa na kuhimiza uwekezaji unaoendana na mahitaji ya jiji

Chalamila amesema mazingira ya hospitali hiyo ni mazuri na yanatoa faraja kwa wagonjwa tofauti na baadhi ya hospitali ambazo wagonjwa huogopa hata kupelekwa kutokana na mazingira yasiyoridhisha.

Amesema lazima watambue eneo lao lina hospitali nyingi ,sasa wanaziunganisha vipi na malengo yenu au mnaziona kama sekta binafsi au sehumu yenu na mwishowe miradi hii itakuwa inajiendesha yenyewe bila kuwa na msaada wa serikali.

Chalamila amesema mtu anaweza kuwa na maono mazuri .lakini kama kuwasapoti hayawezi kutekelezeka yanapaswa kuwa na sera nzuri nanzisizo badilika badilika.

‘Ninayo furaha sana mheshimiwa Rais ameendelea kuwa balozi ,katikanmaswala yanayohusu afya ya mwanadamu na katika hili ameleta mpango wa pamoja wa bima ya fya kwa wote.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kuhamasisha uwekezaji wa hospitali binafsi na kuboresha huduma za matibabu, ili kuongeza imani ya wananchi na wageni wanaohitaji huduma
za kibingwa.

“Nataka Dar es salaam iaminike kwenye matibabu mtu akisikika yuko Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu aaminike kweli anatibiwa,” amesema.

Amesema Hospitali ya Shifaa ni miongoni mwa uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi wenye thamani ya dola milioni 60 uliotekelezwa kwa kushirikisha kampuni za mafuta kupitia Oil Company Group, hatua iliyosaidia kutekeleza maono ya marehemu mzee Bashir aliyekuwa na wazo la kuanzisha uwekezaji huo wa afya.

Amesema katika taifa la leo ,hata ungekuwa na rasilimali nyingi kiasi gani kama huna rasilimali watu wenye uwezo walio salama taifa hilo liko hatarini kwa hiyo ongezeko la hospitali linathibitisha usalama wa uraia katika masuala ya afya zao.

Mwakilishi wa hospitali hiyo, Hilda Bashir amesema ni furaha kubwa mkuu wa mkoa kutembelea hapa kwasababu shifaa ni mshirika mkubwa wa serikali katika kuboresha afya wilaya ya Kinondoni

Hilda amesema uwekezaji huo ,umegharaimu kiasi cha dola za kimarekani sh 60 milioni kwa lengo la kuunga juhudi za serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Amesema uwekezaji wa hospitali hiyo, yenye gorofa tisa una vifaa vya kisasa ,madaktari bingwa 30 , wafanyakazi 1500 na vitanda 250

Mstahiki meya wa manispa hiyo Songolo Mnyonge amesema , hospitali hiyo ni ya kisasa ipo katika manispaa ya kinondoni ina faida ya huduma sio Tanznia pekee na nan je ya anzania

‘’Sisi kama kinondoni tunajivunia hospiutali hii tunayo maeneo 36 ya kutolea huduma lakini hayatoshi kwa hiyo wanapojitokeza wadau kaamhawa kuunga mkono jitihada za serikali tunaendelea kufarika sana Imani yangu watafika katika mikoa mingine’’amesema.

Mganga mkuu Emanuel Maganga, amesema ni jambo la furaha kwao kama Serikali kuja kungalia watoto wao wanakwenda vipi katika utoaji wa huduma kwani wao ndiyo waratibu na watunga sera madhubuti zenye kuvutia wawekezaji.