
Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Pemba
Mgombea ubunge Jimbo la Kojani, Hamad Chande amesema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema Samia Suluhu Hassan amewafanyia mambo makubwa yakiwamo ya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Pemba na barabara.
Chande ametoa kauli hiyo leo Septemba 20,2025 alipopewa nafasi ya kuzungumza katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani Pemba.

Amesema Rais samia amepeleka zaidi ya Sh bilioni 886, huku ujenzi wa Bandari ya Wete, Shumba amepeleka Sh bilioni trilioni 1.26
kwa mema ambayo umefanyia mama tunaambiwa na wasomi kwamba aliyekufanyieni mema mlipeni aliyokufanyie, mkikosa bas muombeni dua na kukulipa kadri ya wema uliotufanyia hatuwezi kusema lolote, tunasubiri Oktoba 29, tunakwenda kutiki.
Mwaka jana nilikuwa na mjomba wangu kwa bahati nzuri au mbaya amefariki, aliniambia mwanangu mwambie Samia kiti cha dereva hakitaliwa na mtu mwingine, wewe tayari kura zako zimefikia pazuri. Kiti cha dereva hata gari likijaa hakikaliwi na mwingine.


