China itaendelea kuiunga mkono Iran katika kulinda mamlaka yake ya kitaifa na heshima, pamoja na kupinga siasa za ukuu na uonevu. Haya yamesemwa leo na waziri wa mambo ya nje wa China kwa mwenzake wa Iran.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang amesema kuwa China inatilia maanani dhamira ya Iran ya kutotengeneza silaha za nyuklia na kuheshimu haki ya Iran ya kutumia kwa amani nishati ya nyuklia.

Wang ameongeza kuwa China iko tayari kuendelea kutekeleza jukumu muhimu la kushinikiza utatuzi wa suala la nyuklia la Iran na kudumisha utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati .

Pia amesema kuwa China inaridhishwa na juhudi za Iran za kufikia amani kupitia diplomasia.