China imekasirishwa na hatua ya serikali ya Marekani kuapa kubatilisha visa za wanafunzi wa China walioko Marekani, ikiita hatua ya Rais Donald Trump kuwa ya kisiasa na kibaguzi.

Awali Marekani ilisema itaondoa nafasi ya wanafunzi hao kuomba visa za kuingia nchini mwake. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning, amesema tayari wamewasilisha malalamishi yao kwa utawala wa Trump. 

Visa za wanafunzi hao zinachangia kiwango kikubwa cha mapato ya vyuo vikuu nchini Marekani.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio amesema taifa lake pia litaimarisha ukaguzi wa visa wa wanafunzi wote kutoka China na Hong Kong 

Marekani imechukua uamuzi huo kutokana na maandamano ya mara kwa mara ya wanafunzi katika vyuo vikuu.