Na Magrethy Katengu,Jamhuri lMedia
Dar es Salaam

CHAMA cha Wananchi CUF kinafanya Mkutano Mkuu Maalum unatarajiwa kufanyika kesho Agosti 9,2025 kwa lengo ni kupitisha wagombea wa Urais.upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliopendekezwa na Baraza kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho uliyofanyika August 6 Mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 8,2025 jijini Dar es slsalaam na Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hiko ambapo amesema wagombea waliopendekezwa kwa upande wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja Gombo Sambandito Gombo na Nkunyuntila Siwale.

Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliopendekezwa kugombea nafasi ya Urais ni Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa,Mhandisi Hamad Masoud Hamad pamoja na Dr.Mohamed Habib Mikidadi ambapo wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum watapiga kura ya kumpata Mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CUF katika kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu.

Hata hivyo Prof. Lipumba amesema katika Mkutano Mkuu huo,CUF itazindua Ilani ya CUF kwa ajili ya kutangaza Sera za chama kwa Wananchi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ili kuwafanya Wananchi waweze kukiamini na kukipa ridhaa ya kushika dola.

“Baraza kuu la Uongozi Taifa limepokea na kupitisha rasimu ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu upande wa Muungano,pamoja na rasimu ya Uchaguzi Mkuu upande wa Zanzibar na kupitisha wagombea wa ubunge,vilevile wagombea wa uwakilishi”amesema Prof. Lipumba.

Aidha amesema kuwa Ilani ya CUF imebeba maono mapana yakujenga Tanzania Mpya kupitia Serikali ya umoja wa kitaifa yenye misingi imara,ya usawa, mshikamano, uwajibikaji, demokrasia ya kweli na Maendeleo jumuishi kwa watu wote.

“Ilani ya CUF imejikita katika misingi yakuweza kuleta haki sawa na furaha kwa Wananchi wote,kujenga uchumi jumuishi unao ongeza ajira na kuondoa umasikini,kuimarisha misingi ya demokrasia na utawala wa Sheria kwa kupata katiba mpya inayotokana na maoni ya Wananchi,kuweka msingi wa maendeleo endelevu kwa kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals) ifikapo mwaka 2030.”amesema Profesa Lipumba.

Nakuongeza kuwa “Ilani yetu inatekeleza Sera ya CUF ya kipato Cha msingi ni haki ya kila Mtanzania kwa kuanza kuwalipa Wazee wote wenye miaka kuanzia 60 nakuendelea kipato cha msingi cha kujikimu,tunaamini kwamba uchaguzi Mkuu ukiwa huru nawa haki Wagombea wanaotokana na CUF chama Cha Wananchi watapata Ushindi kwenye Uchaguzi huo”.

Sambamba na hayo Profesa Lipumba amesema wameridhishwa na mabadiliko yaliyofanywa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiwemo kuvipatia vyama vya siasa nakala halisi ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura, hatua ambayo itasaidia mawakala kutambua idadi na majina kamili ya wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.

Aidha chama hiko kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa Job Ndugai kilichotokea ghafla Agost 6.Mwaka huu.

“Chama cha CUF tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo Cha Job Ndugai Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa pamoja na tofauti zetu zaki itikadi,Kisiasa,tuna tambua kuwa Marehemu alikua Mzalendo,” Amesema Prof Lipumbaa

CUF inawapa pole familia na ndugu wa Marehemu Job Ndugai na Wananchi wa Kongwa na Watanzania kwa ujumla hususani wale wote waliokua wanachukia kuiuza nchi kwa bei poa.

Aidha Bwana alitoa sasa ametwaa Jina lake Libarikiwe na apumzike kwa Amani mpendwa wetu Amina.”amesema kwa huzuni Prof. Lipumba.