Mahakama Kuu ya Anuradhapura, Sri Lanka, imemkuta na hatia daktari mwenye umri wa miaka 70 kwa kosa la kumdhalilisha kijinsia mwanamke mwenye umri wa miaka 25.
Tukio hilo lilitokea baada ya mama huyo kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya kuondolewa kitanzi cha uzazi kilichokuwa kimepandikizwa mwilini mwake, ambapo daktari huyo alitumia nafasi hiyo kumdhalilisha kijinsia.
Hakimu alimhukumu kifungo cha miaka 15 jela na kulipa fidia ya shilingi milioni 1.5.Mahakama pia imeeleza kuwa iwapo mshtakiwa atashindwa kulipa fidia hiyo basi ataongezewa kifungo cha miaka mitatu.
