Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa Sekta ya Afya na TAKUKURU, Mhe. Aswege Enock Kaminyoge, Mkuu wa Wilaya ya Bunda ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi katika warsha hiyo, amewaasa wadau hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU wakati wote kwa manufaa ya jamii inayopata huduma.
Pia amewataka inapobidi waombe msaada wa kufanyiwa uchambuzi wa mifumo ya utendaji kazi ili kubaini mianya ya rushwa iliyopo na kuchukua hatua stahiki mapema.
Aidha aliipongeza TAKUKURU na Menejimenti ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda kwa kuwa kielelezo tosha cha ushirikiano wa sekta binafsi na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.



