BEI ya dhahabu imepanda kwa zaidi ya dola za kimarekani 5,000 (£3,659) kwa gramu 28.35 kwa mara ya kwanza, ni ongezeko la thamani kwa zaidi ya asilimia 60 mwaka 2025.

Hii inakuja huku mvutano kati ya Marekani na NATO kuhusu Greenland ukiongeza wasiwasi kuhusu fedha na siasa.

Sera za biashara za Rais wa Marekani Donald Trump pia zimetia wasiwasi masoko. Siku ya Jumamosi alitishia kuitoza Canada ushuru wa asilimia 100 ikiwa itaingia makubaliano ya kibiashara na China.

Dhahabu na madini mengine ya thamani huonekana kama mali salama ambapo wawekezaji hununua wakati wa wasiwasi katika biashara.

Mahitaji ya madini ya yamechochewa na mambo mengine mbalimbali ikiwa ni pamoja na mfumuko wa bei, dola dhaifu ya Marekani, manunuzi ya benki kuu kote ulimwenguni na huku Hifadhi ya Shirikisho ya Marekani ikitarajiwa kupunguza viwango vya riba tena mwaka huu.

Vita nchini Ukraine na Gaza, pamoja na Washington kumkamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro, pia vimesaidia kuongeza bei ya dhahabu.