Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, Dar es Salaam
DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala, Magreth Cheka, pamoja na Baraza la Umoja Wanawake UWT Kata ya Kipawa ,wamesherekea siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa misaada ya vyakula kwa Watoto wa mahitaji Maalum wa kituo cha ZIli House Children care.
Akiongoza Baraza la Wanawake wa UWT Kipawa pamoja na Diwani wa Kata Kipawa Yusuph Lima ,Diwani Magreth Cheka amesema ziara yao katika kituo hicho cha Watoto wa Mazingira Magumu pamoja na Wanawake wa UWT wamefarijika sana kutembelea kituo hicho kutoa misaada sambamba na kushiriki kazi za kijamii.
“Sisi Wanawake wa UWT Wilaya ya Ilala tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na sisi Wanawake wa wa UWT tunazimisha siku ya Wanawake Duniani ngazi ya kata kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na kutembelea makundi maalum ambapo tumeongozana na Kamati ya Utekelezaji Kipawa pamoja na Baraza lote la UWT na Diwani Mlezi Yusuph Lima ” amesema Cheka.
Diwani Cheka amesema yeye ni Diwani wa viti Maalum Wilaya ya Ilala Wanawake majukumu yake kushughulika na masuala ya Wanawake pamoja na kusaidia makundi maalum.
Kwa upande wake Mlezi wa Kata ya Kipawa Diwani Yusuph Lima amesema yeye ndio mlezi wa kituo cha watoto yatima sababu kipo ndani ya kata ya Kipawa changamoto za kituo hicho atazitatua kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Diwani Lima amesema kituo hicho cha Zili House Children care kina wanafunzi wa shule za awali na shule ya sekondari yeye kama serikali milango ipo wazi atawanulia vifaa vya Saloon wawe wanatumia ikiwemo kujifunza baadae iwe sehemu yao ya kutengeza ajira
Katibu wa UWT Kipawa Habiba chapa ,amesema uwt kipawa wameanza ziara hii kuanzia Tarehe moja Machi wanashiriki kazi mbali mbali za kijamii ngazi ya kata na mtaa katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani.
Mwenyekiti wa UWT Kipawa Praxeda Mkandara, amesema katika ziara hiyo ya Siku ya Wanawake wameongozana na Kamati ya Utekelezaji wa kata pamoja na Baraza la Umoja Wanawake UWT kipawa ,Kata ya Kipawa ina mitaa sita wanawake wa UWT Kipawa wote wameungana na mwanamke mwezao Dkt Samia Suluhu Hassan katika wiki hii ya Wanawake.



