Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutekeleza kikamilifu ahadi yake ya kutoa ajira zaidi ili kuimarisha Jeshi la Uhifadhi nchini.
Akizungumza wakati wa Mahafali ya Kuhitimu askari wapya 256 wa Malaka ya Wanyamapori (TAWA), Dkt. Abbasi amesema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita jumla ya askari 992 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali za uhifadhi.
“Katika eneo hili la ajira Serikali ya Dkt. Samia imetimiza wajibu wake kikamilifu ambapo pamoja na hawa leo wanaohitimu na wanakwenda moja kwa moja kuanza kazi, mwaka jana tumeajiri askari 992 lakini hivi sasa tayari tunavibali vya askari wengine 700 wa taasisi hizi,” alisema.
Hafla hiyo imefanyika leo Februari 2, 2026 katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi, Mwanza.









