📌 Tanzania, Morocco wakubaliana kuimarisha ushirikiano

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko Mei 15, 2025 ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.

Akiwa Bungeni hapo, Dkt. Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika Mhe. Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco.

Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Viwanda na Biashara