*πNi vya Kuongeza msukumo(pressure) wa mafuta PS-5 na kambi ya kuhifadhi mabomba namba 10
*π Ujenzi wa kituo cha kupunguza kasi ya mafuta wafikia asilimia 41
π *Apongeza uwepo wa wazawa kwenye shughuli za mradi ikiwemo wanawake
Na Neema Mbuja, Igunga
Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati Dkt James Mataragio, leo 26 Julai, 2025 ametembelea kituo namba 5 cha kupunguza kasi ya mafuta kilichoko wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora pamoja na kambi namba 10 ya kuhifadhia vifaa vya mabomba ya mradi ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki- EACOP.
Dkt Mataragio amesema kuwa mradi huu ni muhimu sana kwa nchi zote mbili na ameridhishwa na hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa kituo hicho ambao umefikia asilimia 41.

ββ Nipende kuwapongeza sana kwa hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa mradi na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati kama ilivyokuwa kwenye mpango wa utekelezajiββ Alisema Dkt Mataragio
Amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kusaidia utekelezaji wa mradi huu na kuwapongeza kwa kuwapa wazawa kipaumbele kwenye utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki – EACOP .
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi Kitaifa kutoka TPDC Asiadi Mrutu amesema kituo hiki cha kupunguza kasi ya mafuta kinatarajia kutumia Umeme toka TANESCO kama Chanzo kikuu na kitakuwa na jenereta zenye uwezo wa kuzalisha Megawati 30.57 kwa ajili ya dharura.
Mradi wa bomba la mafuta ghafi la EACOP linatarajia kuwa na vituo 6 vya kupunguza kasi ya mafuta ghafi yanayotoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani- Tanga vitakavyojengwa ili kusaidia upunguzaji wa kasi ya mafuta ghafi yanayosafirishwa sambamba na kulinda miundombinu ya bomba hilo la mafuta.

Amesema kwa upande wa Tanzania vituo hivyo vinajengwa maeneo ya Muleba, Mbogwe, Igunga na Singida na vingine viwili vitakuwa nchini Uganda.
Akiwa kambi namba 10 Dkt Mataragio alitembelea eneo la kuhifadhi mabomba na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika lwenye eneo hilo.



