Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amelipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa jitihada kubwa za kulinda maliasili na kuvitangaza vivutio vyake vya utalii ndani na nje ya nchi na kuiheshimisha nchi yetu kimataifa.

Pongezi hizo amezitoa leo Julai 15, 2025 jijini Arusha alipozuru banda la TANAPA lililopo katika Mkutano wa Pili wa Baraza la Vyombo vya Habari Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC – Arusha.

Aidha, Dkt. Mpango aligusia kuwa ushindi wa TANAPA wa tuzo hizo saba (7) za kimataifa za utalii zilizotolewa na Taasisi ya World Travel Awards ni ishara ya kujitoa na uaminia mkubwa ambao shirika hilo la Umma limeendelea kuufanya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1959 chini ya Muasisi wa Taifa hili Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.