Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Dar es Salaam
Licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali kudhibiti ugonjwa wa Saratani lakini bado ugonjwa umeendelea kuongezeka siku siku ambapo takwimu za Mwaka 2022 zaidi ya watu milioni 20 Duniani wamegundulika wana Saratani huku Milioni 9 wakipoteza maisha kila mwaka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo jijini Dar es Salaam Februari 4,2026 Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road Dk Diwani Msemo katika siku ya Maadhimisho ya Saratani Duniani na uzinduzi wa Mashine ya Pet Scan iliyogharimu Bilion 18 ambapo mashine hiyo imesaidi kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanasafiri kwenda India kwa matibabu hivyo kwa sasa watatibiwa nchini .
“Ugonjwa wa Saratani ni tatizo Duniani inahitaji kushughikiwa na hakuna mpaka lazima Mikakati ya kidunia wekwe na kufanya tathimini ya hali halisi ili kusaidia Wananchi wetu wasipoteze Maisha” Amesema Dkt Msemo
Hata hivyo amebainisha kuwa Ugonjwa wa Saratani ni Matibabu yeke ni gharama Sana hivyo Kupitia Bima ya Afya iliyozinduliwa na Serikali yaTsh 150000 kwa kila kaya yenye watu sita inakwenda kuleta suluhisho hivyo ni vyema kila Mtanzania akajiunga na Bima hiyo.



