Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 24, 2026 amekagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani unaotekelezwa katika eneo la Bondeni City katika Halmashauri ya Jiji la Arusha. 

Mradi huo ambao utagharimu shilingi bilioni 14.3 una lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji na kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Arusha.

Mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika Mwezi Mei 2026 umefikia asilimia 49.