Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhi tunzo ya heshima Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ofisi ya Zanzibar, Mhe. Khatibu Mwinyichande aliyotunukiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa kuthamini mchango wake katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kuanzia mwaka 2008 hadi 2013.
Hafla ya kukabidhiwa tunzo hiyo ilifanyika wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya na la kisasa la Afisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) lililopo Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi, leo tarehe 16 Julai 2025.
