Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa( IMF) , Bw. Adran Ubisse ( wa pili kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika makao makuu ya IMF, jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Abebe Selassie, Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine Bw. Abebe amemmwagia sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kusimamia vema sera za uchumi na fedha za nchi yake ikiwemo kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na namna anavyosimamia fedha za miradi zinazotolewa na Taasisi hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa( IMF) , Bw. Adran Ubisse, baada ya kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo katika mazungumzo yao Bw. Ubisse aliipongeza Tanzania kwa kuwa na rekodi nzuri ya utekelezaji wa miradi kwa kutumia vizuri fedha inazokopa.