Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Oktoba 02, 2025 anaendelea kusaka kura za Ushindi wa Kishindo za Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge kwa kufanya mikutano ya hadhara ya Kampeni Mtwara Vijijini.

Dkt Nchimbi mara baada ya kuwasili ameanza mkutano wake wa kwanza kwa kuwasalimia wananchi wa kata ya Nanguruwe, jimbo la Mtwara Vijijini mkoani humo, huku akipokewa na Wananchi kwa shangwe na nderemo.

Baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Mtwara Vijijini,Ndugu Arif Suleiman Premji pamoja na Madiwani.

Dkt. Nchimbi anafikisha mkoa wa 16 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,huku akinadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030 kwa Wananchi