MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya ya Mariadhiano na Amani Tanzania Mkoa wa Katavi (JMAT) leo Jumatano Septemba 10,2025 mjini Mpanda ,Katavi.
Mazungumzo yao yalijikita kuangalia jinsi gani ya kuendeleza amani na mshikamano wa wananchi wa mkoa wa Katavi hasa mnamo kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.
Balozi Dkt.Nchimbi yuko Mkoani Katavi akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni ya kusaka kura za Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pichani akiwa na viongozi hao mara baada ya kikao hicho kwenye ukumbi wa hotel ya Home Ground mjini Mpanda.
