Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, leo Septemba 7, 2025, ameruka kwa helikopta akizisaka kura za kishindo za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Balozi Dk. Nchimbi ameanza ziara yake ya kampeni Mkoani Kagera kwa kishindo, ambapo atafanya mikutano katika maeneo ya Ngara, Kyerwa, Katoro-Bukoba Vijijini na kuhitimisha kwa mkutano mkubwa Bukoba Mjini.

Katika mikutano hiyo, Dk. Nchimbi atanadi sera na Ilani ya CCM, akieleza mikakati na mipango ya chama hicho endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza kwa miaka mitano ijayo.