Mgombea ubunge Jimbo la Songea Mjini, Dk.Damas Ndumbaro amemuomba mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan aendelea kutoa mbolea ya ruzuku Kwa wakulima.

Amesema wakulima wanaomba ruzuku ya mbolea iendelee kwa sababu wameondokana na adha hiyo.

Akizungimza na maelfu ya wananchi kwenye viwanja vya Veta wakati mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu Septemba 21,2025, Dk. Ndumbaro amesema ruzuku hiyo itasaidia wakulima kuondokana na changamoto.

Amesema Rais Samia amefanya kazi kubwa na kwa mara ya kwanza mji wa Songea umepata taa za kuongezea magari.

Amesema wananchi wanashukuru kupata fidia tano katika maneno ya EPZ,barabara ya Songea
-Makambako na uwanja wa ndege wa Songea.

Amesema wanashukuru kwa Ilani mpya ambayo imesheheni vipaumbele vya maendeleo.

“Wana Songea wanashukuru kumleta Ndumbaro kwa ajili ya ubunge.

“Nakushukuru uliniami kwenye baraza lako la mawaziri tangu uliposhika usukani”

Amesema wananchi wa mji huo, wanaomba ujenzi wa barabara ya Bypass ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari katika mji wa Songea.