Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa maji wa Butimba mkoani Mwanza tarehe 20 Juni, 2025. mradi huu wa maji una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 48 kwa siku na hivyo kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Mwanza kwa kuwanufaisha wakazi wa wapatao 450,000 katika maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Lwanhima, Fumagila, Sahwa, Igoma, Kishiri na Nyamhongolo.