Dk Samia akutana na vijana wa kitanzania wanaoishi Oman na kutangaza utalii Duniani ‘Royal Tour’
JamhuriComments Off on Dk Samia akutana na vijana wa kitanzania wanaoishi Oman na kutangaza utalii Duniani ‘Royal Tour’
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa Vijana wa Kitanzania wanaoishi Nchini Oman ulioongozwa na Kiongozi wa Ujumbe huo Khalid Al Barwani ulioshiriki katika ziara ya nchi 9 Duniani katika kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kutangaza Utalii Duniani (Royal Tuor), walipofika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 22 Januari 2026.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mawasiliano, Uchukuzi na Teknolojia ya Habari wa Oman Mhe. Said bin Hamoud Al Maawali Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 22 Januari 2026.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ufunguo wa Gari aina ya (Wrangler Geep) iliyotumika katika ziara ya nchi 9 Duniani katika kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kutangaza Utalii Duniani (Royal Tuor) Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 22 Januari 2026. Anaekabidhi Funguo ni Kiongozi wa Ujumbe huo Khalid Al Barwani.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Funguo ya Gari aina ya (Wrangler Geep) Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abass iliyoshiriki katika ziara ya nchi 9 Duniani kuunga mkono Juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kutangaza Utalii Duniani (Royal Tuor), Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 22 Januari 2026.