Dk Samia ashiriki Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC jijini Arusha
JamhuriComments Off on Dk Samia ashiriki Mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. William Somoei Ruto kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 07 Machi, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. William Somoei Ruto pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 07 Machi, 2026.. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. William Somoei Ruto, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud, Waziri Mkuu wa Rwanda Mhe. Dkt. Justin Nsengiyumva wa pili kutoka (kulia), Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bi. Veronica Nduva wa kwanza (kushoto) pamoja na Viongozi wengine mara baada ya kushiriki katika Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 07 Machi, 2026.