Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha mkoani Arusha leo Oktoba 2, 2025, ambapo amepokelewa na mapokezi makubwa kutoka kwa maelfu ya wananchi waliokusanyika Viwanja vya Mashujaa.

Wananchi wameonekana wenye furaha isiyo kifani, wakipiga makofi, kuimba nyimbo za shangwe na kushangilia uwepo wa Rais Dkt. Samia. Bendera za CCM zilikuwa zikipulizwa kwa nguvu huku sauti ya shangwe zikisikika kila pembe ya viwanja hivyo ikionesha hamasa kubwa ya wananchi.

Dkt. Samia, akiwa katika safari yake ya kampeni, anatarajiwa kunadi Ilani ya CCM, Sera na Ahadi zake, pamoja na kuomba ridhaa ya wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla ili kuendelea kuongoza Taifa kwa miaka mitano ijayo ifikapo Oktoba 29, 2025.