Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Watanzania wametakiwa kuzingatia mpangilio mzuri wa lishe bora ili kuimarisha afya ya mwili sambamba na kuongeza kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo yameshamiri kutokana na mtindo mbaya wa maisha na ulaji usiofaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Daktari Mkuu wa Kampuni ya Norland kwa Afrika Mashariki inayojihusisha na utafiti, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za tiba mbadala yenye Makao yake Makuu nchini China, Dkt. Moses Makalla alisema kuwa elimu kuhusu lishe bora bado haijawafikia Watanzania wengi.
“Kukosekana kwa elimu ya kutosha kunachangia ongezeko la magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani, magonjwa ya figo, moyo na mengineyo,” alisema Dkt Makalla na kuongeza kuongeza kuwa watu wengi wanakumbwa na magonjwa haya kwa sababu ya ulaji usiofaa na maisha yasiyo na mpangilio mzuri.
kwa mujibu wa Dkt Makalla, elimu ya lishe ni muhimu sana kwa afya ya jamii na kwamba Norland mbali ya kuja na suluhisho la kutibu chanzo cha tatizo pia wanatoa elimu ya lishe bora.
“Bidhaa zetu zimeidhinishwa na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) na zimeonesha mafanikio makubwa kwa wagonjwa wa ndani na nje ya nchi,” alieleza Dkt. Makalla.
Aidha, alisisitiza kuwa kila kundi la umri lina aina yake ya mahitaji ya chakula na haishauliwi kula chakula kwa mazoea bila kuzingatia umri, hali ya afya au mahitaji maalum ya mwili.
Katika kutoa ushauri kwa wanawake wanaotafuta ujauzito, Dkt. Makalla aliwataka kuzingatia lishe yenye virutubisho sahihi na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye wanga na sukari nyingi, ambavyo ni hatari kwa mfumo wa uzazi.
Kutokana na ukubwa wa tatizo la magonjwa yasiyoambukiza, Dkt. Makalla alisema Norland imekuwa ikitoa elimu ya mtindo bora wa maisha ili kupunguza maambukizi na vifo vinavyotokana na magonjwa haya.
“Tangu mwaka 2019, tumekuwa tukitoa huduma hizi katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam ambayo yameathiriwa zaidi na magonjwa hayo na kuongeza kuwa Norland ina mpango wa kupanua huduma hkatika mikoa yote nchini nzima.
Akizungumzia zaidi umahiri wa bidhaa zao sokoni na mafanikio waliyoyapata watumiaji, Dkt. Makalla alisisitiza kuwa bidhaa za Norland hutibu chanzo cha tatizo badala ya kushughulikia dalili pekee.
Alitoa wito kwa wananchi kubadilisha mtindo wa maisha kwa kuzingatia lishe bora na kusoma au kushauriana na wataalamu wa afya ili kujifunza zaidi kuhusu mlo unaofaa.
