Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ameapishwa na kula kiapo cha uaminifu na ahadi ya uzalendo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu mara baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

‎Mhe. Dkt. Gwajima ameahidi, kulitumikia taifa kwa moyo wake wote.

Katika kipindi cha mwaka 2020-2025 Dkt. Dorothy Gwajima aliteuliwa kuwa mbunge na alihudumu kama Waziri wa Wizara mbili ambazo ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (2020–2022) na baadaye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (2022–2025).