UMOJA wa Ulaya (EU) unatarajiwa kuidhinisha awamu mpya ya vikwazo dhidi ya Urusi ikiwa ni hatua nyingine ya kushinikiza Kremlin kusitisha uvamizi wake dhidi ya Ukraine.

Hatua hiyo imecheleweshwa kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na upinzani kutoka Slovakia, ambayo serikali yake ina uhusiano wa karibu na Moscow .

Slovakia inapinga uamuzi wa EU wa kuachana kabisa na matumizi ya gesi ya Urusi kufikia mwaka 2028, ikitaka fidia ya kiuchumi kabla ya kuunga mkono mpango huo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Brussels, kifurushi hicho kipya cha masharti 18 kitaimarisha vikwazo vilivyopo dhidi ya wanunuzi na wasafirishaji wa bidhaa za mafuta kutoka Urusi.

Pia, kitapanua hatua hizo kwa kuzilenga benki za Urusi pamoja na kampuni kutoka China na Belarusi zinazoshutumiwa kuisaidia Urusi kukwepa vikwazo vya Ulaya.