Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Tume ya Ushindani (FCC) imesema kuwa itaendelea kuchukua hatua katika
kuhakikisha walaji wa bidhaa na huduma wanapata salama zinazokidhi viwango.
Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Khadija Ngasongwa wakati akitangaza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Mlaji Duniani ,jijini Dar es Salaam.
Ngasongwa amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Mlaji huadhimishwa kila mwaka machi 15 na kilele chake machi 31 kwa Kwa Kauli mbiu Bidhaa salama, Imani kwa Mlaji.
Amesema kupitia kaul mbiu hiyo inalenga umuhimu wa kuhakikisha kuwa bidhaa na zinazotolewa sokoni ni salama zenye viwango vinakubalika kitaifa au Kimataifa na hazihatarishi afya,usalama au maslahi ya mlaji.
Amesema kuwa siku ya mlaji ni lujrnga imani ya walaji katika soko kwa kuhakikisha uwazi ,ubora na uwajibikaji kwa wafanyabiashara.
Amesema katika kauli ya mwaka huu zimekuwa nyingi ya kwanza inasema
mlaji mwenye kuzingatia suala la ubora huchangia ukuaji wa uchumi imara na pili kwa sababu ya kuchagua bidhaa na huduma zenye ubora Wafanyabiashara wanaozalisha na kusambaza bidhaa bidhaa bora hunufaika
na mazingira ya ushindani wa haki jambo linalochochea ubunifu na ufanisi na hatimaye kukua kwa uchumi.
Ngasongwa kufuatia na maadhimisho hayo FCC itatoa elimu kwa wadau mbalimbali katika kuendelea kulinda soko la ushindani nchini.
Aidha amesema kuwa kazi kubwa itatofanyika ya kutoa elimu kwa wananchi
wa kuendelea kupata bidhaa na pamoja huduma zilizo bora.


