Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

TUME ya Ushindani (FCC) imewataka waandishi wa habari nchini,kutumia
kalamu zao kupaza sauti ili watu wafahamu kazi za FCC na kukuza uchumi

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, amesema kuwa tume hiyo ina utaratibu wa kukutana na wadau wake mara kwa mara ili kujadili masuala yanayohusu ushindani wa soko.

Amesema Waandishi wa Habari wakijua majukumu ya FCC ,wataweza kuelimisha jamii juu ya kazi za FCC kwa kuwa wao wana nafasi ya kuchunguza mambo mbalimbali.

‘’Kazi inaweza kuingia kwenye jamii na kuchunguza jambo na mkapata ukweli wa hilo jambo ambalo sisi kama fcc tukiona mwandishi ameweza kuibua jambo inaturahisishia kufuatilia’’amesema

Amesema maantiki hiyo FCC itaweka , mazingira wezeshi ili waandishi eaweze kutoa michango yao itakayo kusadia kutekeleza sheria za ushindani na alama za bidhaa.

‘’Tuna marajio mtajifunza maswala mbalimbali ya sheria zinazohusu FCC,
ili kuona hakuna bidha bandia zinazoweza kuingia nchini.

Sheria ya alama za bidhaa inahusika na kuangalia ubora bidhaa, ambayo tuna mashaka nayo wa bidhaa kimsingi.

Kama waandishi wa habari lengo la semina hii muendelee kuisadia Serikali kwa sababu mchango wenu mkubwa sana’’amesema.

Amesema majukumu makubwa ya FCC ni kumjua mzalishaji na msambazaji na
hii inaturahisishia kufanya majukumu yetu pale hasa tunapotaka kumfuatilia kujua kila kitu tangu mpaka bidhaa inapoingia sokoni

‘’Kwa sasa , majuku yetu yameingiliana baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya sheria mwaka jana ambayo sisi katika bunge tuliweza kupeleka mabadiliko na tukapata nafasi ya kurekodi alama za bidhaa kwa
lengo la kuwalinda walaji.

‘’Bidhaa nyingi zinazoingizwana zinazotengenezwa na kuagizwa nje ya
nchi ndiyo zinasajiliwa brella lakini kuna baadhi ya vitu ili kusimamia maslahi ya walaji Bidhaa tunazirekodi ili kuweza kutusadai
kuzirinda kwani inatuwezesha kumfahamu bidhaa, mtengenezaji, msambazaji ,wakala na hivyo tunaweza kunatambua mnyororo mzima wa thamani’’amesema .

Amesema sheria ya ushindani inawarahisishia kufuatilia kwa karibu na
kujua bidhaa inapoingia sokoni muhusika ni nani na hapo tunapata rekodi kama watu wanalalamika kwamba bidhaa haijakidhi viwango au kuna kitu kimeharibika hakiko sawa.

Amesema FCC ina sera inayohusu mtu kurejeshewa gharama zake kama
amenunua kitu ambacho hakija kidhi viwango ,tunamsadia tunamwandikia
mwenye duka na tunawaweka pamoja wanamalizana

Aidha tuna mifumo ya sheria ,ambayo wameitengenezea kanuni zake ambazo bado zina andaliwa kuhakikisha pale wasipokubaliana kama taasisi
inayomlinda mraji

Amesedai kwenye mifumo ya TANOGA a inawezesha ,kungalia bidhaa zinazopitia forodha hii mifumo iko chini ya tra kwa zile taasisi ambazo hazina mifumo yake ya ndani yakungalia bidhaa zinazoingioa

Amesema mamlaka ya mapato waimetengeneza mifumo hiyo kwa tasisis za
serikali kwa lengo la kwamba kama unafanya ukaguzi ufanyike kwa wakati ili isaidie mizigo isirundikane kule ndani

‘’Kwetu sisi ni jambo la muhimu sana ,kwani tutakuwa tunaendena na matakwa ya muheshimiwa rais anataka mifumo isomane na inaposomane
inatusadia kufanya kazi kuwa rahisi na ufanisi kwa kupunguza mizigo ya wafanya biashara ambao mwisho wa siku akipata changamoto wakati wa kuingiza ile gharama anaihamishia kwa walaji.

Kwa hiyo lengo hilo na sisi tunatilia mkazo ,kwa maana ya kwamba ndiyo litakalo tengenezea tija tukaona ni vyema tuwaite waandishi ili na nyinyi muweze kufahamu namna fcc tunavyoweza kutekeleza kipengele hicho kuweza kuishi katika maono ya rais’’amesema

Amesema shabaha ya semina hiyo ni kwenda kutekeleza sheria ya ushidani ya mwaka 2003 na sheria ya alama za bidhaa ya mwaka 1963 hii ni sheria mama inayothibiti bidhaa bandia inafanyiwa marekebishohicho kipengere cha kurekodi kwa maana ya kuweza kuitambusa bidhaa
inapozalishwa mpaka inapokwenda

Kuna baadhi ya maboresho tunafanya, ili kuweza kuzipa nguvu sheria hizi ziweze kutekeleza majukumu yake ili kusiwepo upotoshaji na kuzibiti bidhaa bandia

Meneja wa muungano wa makampuni Innocent Swati amesema muungano wa
makampuni ni kitendo cha kampuni moja kununua ingine, sheria ya ushindani inatasiri kama muungano wa pamoja.

‘’Kikubwa tunachokingalia ni uwezo wa kampuni inayonunua ingine kwakuwa inavunja uhuru wa kampuni ingine uliokuwa nao kabla ya huo muungano’’amesema.

Swati amesema uzibithi wa makampuni .unazibiti makampuni makubwa lakini sio yale madogo nakati wale wanakwenda sehemu nyingine .

‘’kwanini tunathibi bidhaa sababu kubwa ni kuthibiti ushindani lengo kubwa kuhakikisha ushindani haupotei kwa faida ya mlaji kwasababu ukikosekana mlaji ndiyo anaumia kwani mtengenezaji anaweza kutengeneza bidha zisizo na ubora na mlaji akawa hana chaguo ndiyo maana tupo’’amesema.

Meneja wa huduma za sheria Josephat Kizungo amesema marekebisho ya
sheria ya ushindani. huzuia matumizi ya mabaya ya hadhi ya soko itokanayo na watoa huduma zaidi ya mmoja kuainisha mienendo ya matumizi mabaya ya hadhi ya soko na kutambua kosa la washindani kugawana masoko au wateja kutambua utaratibu wa nafuu ya adhabu.

Kizungo amesema kubadili wigo wa hadhi ya soko kutopka asilimia 35 hadi 40 kuruhusu miungano ya kampuni bila ukomo kwa kuzingatia maslahi ya umma.