Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa, amesema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu wananchi wanapaswa kuchagua mgombea anayejua mahitaji yao na mwenye uwezo wa kuyatatua.
Ameyasema hayo Oktoba 3, 2025, katika muendelezo wa kampeni za Mgombea Urais wa Chama hicho.
Aidha, amebainisha kuwa majukumu makuu ya Serikali ni mawili ambayo ni kulinda na kutunza amani, usalama na mshikamano wa kitaifa pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweza kulinda na kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa taifa, jambo ambalo ni msingi wa shughuli zote za wananchi na viongozi wa dini.
Aidha, amebainisha kuwa Dkt. Samia amechukua hatua za kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa ambapo ukuaji wa uchumi umepanda kutoka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 6 mwaka huu.
Pia, amesema kuwa hatua hizo zimekwenda sambamba na kudhibiti mfumuko wa bei ili kupunguza gharama za maisha, hasa katika bidhaa muhimu kama mchele, mahindi na maharage ambazo bei zake zimebaki sawa kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.
Aidha, amesema kuwa changamoto ya bei ya mafuta duniani baada ya vita ya Ukraine ilisababisha kupanda kwa gharama, lakini Dkt. Samia alitoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 ili bei ya mafuta ibaki katika kiwango kilichokuwepo, hatua ambayo Tanzania pekee katika ukanda wa Afrika iliweza kuchukua.
Pia, amebainisha kuwa Dkt. Samia ametoa ruzuku ya shilingi bilioni 693 kwa wakulima milioni 2.2 wakiwemo wa Arusha kwa ajili ya mbolea, sambamba na kutoa shilingi trilioni 1.308 ili kuondoa ada kwa shule za msingi hadi sekondari. Aidha, ametoa shilingi trilioni 2.607 kwa mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ili kuhakikisha hawafukuzwi kwa sababu ya ada, hatua iliyopunguza gharama kwa wazazi.
Aidha, amesema kuwa Rais Samia amepeleka umeme vijijini na kupunguza gharama ya kuunganishiwa kutoka shilingi laki nne hadi shilingi elfu 27 pekee. Huku akibainisha kuwa, Dkt. Samia ameelekeza kushusha bei ya mitungi ya gesi kutoka shilingi elfu 14 hadi 6 ili kuongeza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.
Pia, amebainisha kuwa gharama za ujenzi zimedhibitiwa, ikiwemo bei ya saruji ambayo kwa miaka minne imebaki kati ya shilingi 18,000.
.





