Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amezindua rasmi Jarida la Uchumi Wetu, Toleo Namba 1 la Julai, 2025 linaloandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kupitia Idara ya Mawasiliano kila baada ya miezi mitatu.
Akizungumza katika uzinduzi wa jarida hilo Gavana Tutuba alipongeza kazi nzuri inayofanywa na Idara hiyo katika kuhabarisha umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania.

Ameongeza kuwa Jarida hilo litakuwa ni wenzo wa kuuwezesha umma kusoma habari zihusuzo sekta ya fedha na uchumi wa nchi kiujumla zinazotoka Benki Kuu, Serikalini pamoja na sekta binafsi.
Jarida la Uchumi Wetu limesheheni maarifa kupitia habari, makala na matukio mbalimbali na litasambazwa kwa njia ya nakala tepe (soft copies) kupitia tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania www.bot.go.tz



