Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI 100 wamesafiri kwenda kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini India kwa mwaka huu wa masomo kupitia Global Education Link.
Meneja Mkuu wa GEL, Regina Lema alisema taasisi hiyo imekuwa na kawaida ya kuwasindikiza wanafunzi hao hadi kwenye vyuo wanavyokwenda na kuhakikisha wanapata malazi.

Alisema lengo ni kuhakikisha wanafunzi wamefika salama na kupata usili chuoni kwani ni humuma ambazo taasisi ya GEL imekuwa ikitoa kwa wanafunzi hao.
Alisema tarehe 10 mwezi wa tisa kundi lingine la wanafunzi 100 litaondoka kwenda nchi za China na Malasyia na watasindikizwa na watumishi wa Global
“Huu ni mwanzo wa wanafunzi kuondoka kwasababu kila baada ya siku 10 wanafunzi watakuwa wanaondoka kwenda nnje ya nchi kwa hiyo mwanafunzi ambaye hujapata udahili kusoma nje ya nchi uje GEL kupata nafasi kwenye vyuo nje ya nchi,” alisema
Regina alisema wamekuwa wakiwapa wanafunzi mikopo isiyo na riba ili kuwapunguzia msongo wa mawazo pale wanapokuwa na changamoto ya kulipa ada.

“Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link aliwapongeza wazazi kwa kuwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kwa kujinyima na kufanya uwekezaji huo.
Alisema Tanzania limefungua milango ya mwingiliano baina ya mataifa mbalimbali na kuongeza kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuleta fursa kutoka maeneo wanakokwenda kusoma
“Tunawaona wahindi wanakwenda kila kona duniani, wachina wanatoka kuja kwenye mataifa mbalimbali kwa hiyo na vijana wetu waone fursa huko wanakokwenda kusoma, ili watanzania wengi wenye changamoto ya ajira wapate ajira nje,”.

“Tunahitaji ajira ajira zinapatikanaje? Kwa hiyo wanafunzi wanakwenda kusoma na watu wa aina mbalimbali kuna matajiri wan chi zilizoendelea watakutana nao kwa hiyo wawe mabalozi wan chi yao kwa kuwakaribisha kuna kutembelea Tanzania,” alisema
“Bodi ya Utalii nchini TTB walikuja waliwaeleza kuwa milango ya uwekezaji imefunguliwa ni kazi kwao kuwa mabalozi kwa kuelezea uzuri wa Tanzania na vivutio vyetu ili watu kutoka mataifa mbalimbali duniani waje kuwekeza hapa nchini,’ alisema.
