Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Namtumbo
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ally Senga Gugu amefungua kituo cha Polisi Cha Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma chenye hadhi ya Daraja B ambacho kimejengwa kwa thamani ya sh. Milioni 798.
Akizungumza wakati akifungua kituo hicho katibu Mkuu huyo Gugu amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa.

Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka minne iliyopita Serikali imejitahidi kuhakikisha inaboreshwa miundombinu kwenye vituo vya Polisi kikiwemo kituo cha Polisi Cha Daraja B ambachokimejengwa kwa mfumo wa kutumia mafundi wa kawaida.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge mambo ya Nje ulinzi na usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Kawawa amemshukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Jeshi la Polisi chini ya IGP Camilius Wambura kwa kuona umuhimu wa kuboresha miundombinu ya majengo ya vituo vya Polisi,vitendea kazi pamoja na kutoa vyeo kwa askari Polisi jambo ambalo linaleta molari kwa askari Polisi nchini na kufanya kazi kwa weledi.





