Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Madagascar baada ya wiki kadhaa za maandamano ya umma dhidi ya utawala wa Rais Andry Rajoelina.
Guterres amekosoa mabadiliko ya uongozi yasiyozingatia katiba na ametoa mwito wa kurejea kwa utawala wa kiraia chini ya msingi wa katiba.
Matamshi yake ameyatoa wakati kanali wa jeshi aliyechukua madaraka siku ya Jumanne Michael Randrianirina anatarajiwa kuapishwa leo Ijumaa kuwa rais wakati wa halfa itakayofanyika katika majengo ya Mahakama ya Juu ya Katiba kwenye mji mkuu, Antananarivo.
Umoja wa Afrika pia umelaani mapinduzi hayo na kuisimamisha Madagascar uanachama wake.
