Mbivu na mbichi za wagombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi ujao kujulikana leo Julai 29,2025 saa nne asubuhi baada ya kazi hiyo kushindwa kukamilika jana kama ilivyokuwa imefahamishwa.
Jana Julai 28,2025 Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM CPA Amos Makala aliitisha kikao na waandishi wa Habari kilichooaswa kufanyika majira ya saa 11 jioni lakini hata hivyo kikao hicho kilishindikana kufanyika kutokana na mchakato wa kuchukua wagombea kutokamilika kama ilivyokuwa imepangwa.
Waandishi wa Habari walisubiri bila kuchoka kutoka jana saa 11 jioni ya Julai 28,2025 hadi saa 10 alfajiri ya Julai 29 walipotaarifiwa na Afisa Habari wa CCM Aboubakar Liongo kwamba kazi bado haijakamikamilika na kuambiwa kikao hicho sasa kitafanyika saa nne asubuhi Julai 29, 2025.
