Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Chama ch Mapindizi (CCM) , Wilaya ya Ilala, imejivunia mafanikio kwa kipindi cha miaka minne chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa wilaya Edward Mpogolo ,mara baada ya uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama mapindizi wilaya Ilala kuanzia Dec 2025 hasi Feb 2026 kilicho jumuisha viongozi mbaimbali wa chama hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Mpogolo amesema taarifa yao imejikita katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasani ambapo katika Wilaya ya Ilala wamefanikiwa Kwa asilimia 85
Amesema halimashauri ya Ilala imekuwa na miradi mingi ,ambayo kwasasa imekwenda kukamilika kwa hiyo hatuna budi kumshukuru Rais kwa mchango wake mkubwa kutokana na fedha ambazo amewapatia wananchi wa Iala.
Kwa upande wa elimu amesema halimashauri yake inafanya jitihada kubwa kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri
Amedai halimashauri hiyo ina zaidi ya watoto laki nne ambao wako katika shule za msingi na sekondari, ambapo changamoto kubwa ni vyumba vya madarasa ..
Amesema kwenye eneo hilo,halimashauri imejikita kuhakikisha kwamba ‘wanaongeza vyumba vingi vya madarasa na madawati kwasababu kutakuwa na ongezeko la watoto mwaka 2028.
“Mwaka huu tumetenga zaidi ya sh.milioni 400 Kwa msingi na sekondari sh.400 milioni ambapo sasa wakandarasi wanakwenda kutengeneza madawati.
Bajeti yetu ya mwaka imetenga zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya madawa hivyo tunakwenda kutekeleza changamoto ya madawati na madarasa.
‘Nawashukuru sana waandishi wa habari , kwa mchango wenu mmekuwa mkiandika taarifa mbalimbali za kuonyesha Rais amefanya kazi kubwa”amesema.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Nurdin Juma ambaye pia ni Diwani wa kata ya mchikichini amesema ndiyo mkutano wake wa kwanza anaonba wajumbe wakapate mafunzo ya pamoja katika chuo cha Dipromasia kwa gharama zake iwasadie kusonga mbele.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapindizi Wilaya ya Ilala Said Side amesema ni vyema viongozi walio chaguliw a ,watengeneze mahusiano mazuri na serikali ili kusukuma gurudumu mbele.



