Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Katavi
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Andrew Mwalugaja, ameendelea kuwa mstari wa mbele katika kuongoza sekta ya madini kwa uwajibikaji, weledi na ubunifu.
Kupitia usimamizi wake, Katavi imepiga hatua kubwa katika kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuongeza kasi ya utoaji wa leseni, kuimarisha usalama na kufungua masoko mapya ya madini.
Uongozi wake umeimarisha ushirikiano kati ya Serikali, wawekezaji na wachimbaji, hatua iliyobadilisha taswira ya Katavi na kuufanya mkoa huo kuwa kitovu kipya kinachoongoza kwa fursa za uwekezaji wa madini nchini.



