IRAN imesema itajibu vikali shambulizi lolote litakalofanywa na Marekani. Ujumbe wa Iran kwenye umoja huo umetoa onyo hilo jana Jumatano likijibu kitisho cha Rais Donald Trump cha kuiingilia kijeshi.
Ujumbe huo uliandika kwenye mtandao wa X kwamba Iran iko tayari kwa mazungumzo ya kuheshimiana na yenye maslahi kwa pande zote, lakini ikaonya ikiwa italazimishwa, itajilinda na kujibu vikali kuliko ilivyowahi kutokea.
Trump juzi alirudia tena kutoa vitisho vya kuishambulia Iran akisema muda unakwenda wa kufikia makubaliano ya nyuklia na kusema, kwa kuwa tayari aliitaka Iran kufikia makubaliano, lakini hawakufanya hivyo shambulizi litakalofuata litakuwa la maangamizi kwa taifa hilo.


