Israel inasema imeanzisha mashambulizi kwenye bandari tatu na kiwanda cha nguvu za umeme katika maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi ya Yemen.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alithibitisha wanacholenga ikiwa ni pamoja na meli ya kibiashara ya Galaxy.
Meli hiyo, iliyotekwa nyara na kikundi cha waasi mnamo 2023, ilitumiwa kufuatilia vyombo vya baharini katika maji ya kimataifa, Israel ilisema.
Baada ya mashambulizi ya Israel kwenye bandari za Hudaydah, Ras Isa na Saif, makombora mawili yalirushwa kutoka Yemen hadi Israel, kwa mujibu wa jeshi la Israel.
Msemaji wa kundi la kijeshi la Houthi linaloungwa mkono na Iran alisema kufuatia mashambulizi hayo, walinzi wa anga wa kundi hilo walikabiliana na shambulio la Israel kwa kutumia “idadi kubwa ya makombora ya kutoka ardhini hadi angani yaliyotengenezwa nchini humo”.
Ving’ora vilisikika katika maeneo kadhaa ya Israel kujibu makombora hayo, huku jeshi likisema matokeo ya uvamizi huo yanachunguzwa.
Vyombo vya habari vinavyoongozwa na Houthi nchini Yemen vilisema mashambulizi ya Israel yalishambulia Hudaydah, lakini hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu uharibifu au majeruhi.
