Waziri Mkuu wa Serikali ya Houthi nchini Yemen, Ahmed al-Rahawi, ameuwawa kwa shambulio la anga la Israel tarehe 28 Agosti 2025. Shambulio hilo lililenga mkutano wa viongozi waandamizi mjini Sanaa na kuua pia mawaziri kadhaa.

Houthi wamethibitisha kifo hicho na tayari wamemteua Muhammad Ahmed Miftah kuwa Waziri Mkuu mpya kuanzia 30 Agosti 2025.

Kifo cha al-Rahawi kimeongeza mvutano kati ya Israel na kundi la Houthi, ambalo limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya Israel na meli katika Bahari ya Shamu likidai kuunga mkono Palestina. Wachambuzi wanaonya hali hii inaweza kuongeza ukali wa mgogoro wa Mashariki ya Kati.