Hukumu imetolewa bila mshitakiwa kuwepo mahakamani

*Mshitakiwa anatafutwa ili kutumika kifungo,baada ya kutokome kusikojulikana

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kagera,

Rweyemamu Kashunja alimaarufu Baba P (35) dereva bodaboda mkazi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani na Mahakama ya wilaya Bukoba kwa kosa la kumlaiwiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano

Hukumu hiyo ilisomwa  na kutolewa Mei 30 mwaka 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya ya Bukoba Frola Kaijage, huku mshitakiwa huyo akiwa hayupo mahakamani hapo kwa madai kuwa ametoroka na mke wake wakati shauri hilo likiendelea baada ya kupata dhamana.

Ambapo mshitakiwa huyo alidhaminiwa na watu wawili,mdhamini wa kwanza alikuwa ni  Anchira Gozbart ambaye ni mke wake ambaye wametotoka naye na mdhamini wa pili ni Nelson Mutaghywa aliyeweka dhama ya milioni 10 yeye amehukumiwa kifungo cha nje miezi sita na kulipa kiasi hicho cha fedha.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Wakili wa Serikali Amon Mang’era, amesema katika kesi hiyo,mtuhumiwa huyo namba moja alikuwa na  wenzake wawili ambao ni watoto wa miaka (14 ) wao walifanya kosa hilo kivyao na sehemu tofauti na Rweyemamu.

Mang’era, amesema wakati muathirika anafanyiwa tukio alikuwa na umri wa miaka ( 5 ) sasa ana miaka ( 6 ),huku tukio hilo likifanyika kati ya Aprili  na Desemba 30,2024.

Washtakiwa wote watatu walishtakiwa kwa kosa la kulawiti na kesi ilianza kusikilizwa Mei 12 mwaka 2025, katika mahakama ya Wilaya ya Bukoba mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Frola Kaijage.

Haya hivyo Mang’era,amesema upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watano na vielelezo viwili, huku akidai kuwa wakati shauri likiendelea mahakamani mshitakiwa wa kwanza ambaye ni  Rweyemamu Kashunja, (aliruka dhamana) kwa  kukimbia na mdhamini wake wa kwanza,ambaye ni mke wake.

Amesema kesi ikiwa inakaribia mwishoni washtakiwa wawili ambao ni watoto walikiri kosa na mahakama ikawatia hatiani na kuwapa adhabu kulingana na sheria ya mtoto sura ya 13 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 na wamekabidhiwa chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii ili wapatiwe ushauri nasaha.

Amesema mshitakiwa wa kwanza ambaye ametoroka, amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kulawiti kinyume na kifungu cha 154 kifungu kidogo ( 1 ) ( A )sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2022.

Hata hivyo amesema mshtakiwa anatafutwa popote atakapopatikana na atakamatwa ili aweze kutumikia adhabu yake sanjari na mkewe ambaye ni mdhamini namba moja.